Mshauri wa Rais wa Tanzania katika masuala ya mabadiliko ya tabianchi Richard Muyungi ambaye pia anawakilisha mataifa ya Afrika katika masuala ya mazingira Umoja wa Mataifa amesema njia pekee ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi ni utekelezaji wa miradi ya kukabiliana na kadhia hiyo kikamilifu.