Muwafaka juu ya katiba mpya Afghanistan:
3 Januari 2004Matangazo
KABUL: Rais wa Afghanistan Hamid Karsai amesema wajumbe wa mkutano wa katiba wamweza kusawazisha tafauti zao na hivi sasa wako karibu ya kufikia muwafaka. Zimekwisha patikana suluhisho kadha, na matatizo mengine yatatanzuliwa hii leo, alisema Rais Karsai mjini Kabul. Ni muhimu kuwa muwafaka wa katiba ufikiwe na wingi mkubwa wa wajumbe,alisema. Lakini inasemekana kungaliko tafauti kubwa bado kuhusu swali la kupewa uraiya wa aina mbili wajumbe wa ngazi ya juu wa serikali. Naye Naibu wa Waziri wa Mambo ya Ndani Abdul-Rahim Wardak alisema swali jengine muhimu linaloendelea kujadiliwa ni lugha rasmi ya kiserikali.