Muungano tawala Benin wamteua waziri wa fedha kuwania urais
31 Agosti 2025Matangazo
Uamuzi uliotangazwa baada ya kikao cha siri nyumbani kwa Rais Patrice Talon, ambaye amesisitiza hatagombea muhula wa tatu kikatiba. Muungano tawala unaundwa na vyama kadhaa, kikiwemo cha Republican Bloc - BR na Progressive Union for Renewal - UP-R. Wadagni, ambaye amekuwa mshirika wa karibu wa Talontangu mwaka wa 2016 na amehudumu kama waziri wa uchumi, anasifika kwa kusimamia nidhamu ya kifedha na kuimarisha uchumi wa Benin uliokua kwa zaidi ya asilimia 6 kwa mwaka, pamoja na kuvutia wawekezaji wa kimataifa.
Anatarajiwa kukabiliana na mgombea wa chama cha upinzani cha The Democrats (LD) kinachoongozwa na Rais wa zamani Thomas Yayi Boni, ingawa chama hicho bado hakijatangaza jina la mgombea wao.