Museveni awania muhula wa saba madarakani
28 Juni 2025Museveni, mwenye umri wa miaka 80, amepuuza wito wa kustaafu huku wakosoaji wake wakionya kwamba amegeuka kuwa mtawala wa kiimla, kwa kuwa hana upinzani wa maana hata ndani ya chama tawala cha National Resistance Movement (NRM).
Rais Museveni alipokelewa na umati mkubwa wa wafuasi alipokwenda kuchukua fomu za uteuzi katika makao makuu ya chama jijini Kampala. Museveni alichukua madaraka kwa mara ya kwanza kama kiongozi wa waasi mwaka 1986, na tangu hapo ameshinda uchaguzi mara sita, ingawa chaguzi za hivi karibuni zimegubikwa na vurugu na madai ya wizi wa kura.
Mpinzaniwake mkuu katika uchaguzi uliopita Robert Kyagulanyi, pia ametangaza nia ya kugombea katika uchaguzi uliopangwa kufanyika Januari 2026.
Tangu kupata uhuru kutoka kwa Waingereza mwaka 1962, Uganda haijawahi kushuhudia mabadiliko ya uongozi kwa njia ya amani.