Munich. Ujerumani. Magari yanayotumia dizeli kupigwa marufuku kuingia katikati ya miji.
29 Machi 2005Matangazo
Suala la vumbi katika miji ya Ujerumani limefikishwa tena katika mahakama.
Kundi moja linalolinda mazingira nchini Ujerumani, Deutsche Umwelthilfe, limesema kuwa kiwango cha chembechembe za vumbi zisizoonekana kwa macho, katika hewa mjini Munich kiko juu kuliko kiwango kinachokubalika na jumuiya ya Ulaya. Kundi hilo linafanya kampeni kuyataka magari yote yanayotumia mafuta ya dizeli ambayo hayana chombo maalum cha kuchujia chembe chembe hizo yapigwe marufuku kutumia barabara katikati ya mji. Miji mingine ya Ujerumani kama Düsseldorf na Berlin pia imeonekana na kiwango kikubwa cha vumbi kuliko kile kinachokubalika na jumuiya ya Ulaya.