MUNICH : Papa aendelea na ziara yake mkoa alikozaliwa
11 Septemba 2006Papa Benedict wa 16 ameondoka Munich kuelekea kwenye mji wa Altötting.
Hicho ni kituo chake cha tatu cha ziara ya Papa kwenye mkoa alikozaliwa wa Bavaria nchini Ujerumani.Baadae leo hii Papa Benedikt anatazamiwa kuelekea katika kijiji alikozaliwa cha Marktl am Inn kilioko mpakani na Austria.
Hapo jana amewataka Wajerumani kurudia tena ahadi zao kwa kufuata maadili ya Kikristo.Alitowa wito huo wakati wa misa ya jioni iliofanyika kwenye kanisa la Liebfrauen mjini Munich.Misa hiyo ilitanguliwa na ile iliofanyika hadharani karibu na kituo cha mikutano mjini Munich iliohudhuriwa na watu 250,00.
Katika misa hiyo Papa Benedikt alionya ulimwengu wa kisasa kutoweka imani yao kwa tekenlojia na sayansi jambo ambalo linawafanya wawe hawasikii ujumbe wa Mungu na amesema kwamba Afrika na Asia ni mfano wa kuigwa na mataifa ya magharibi juu ya namna ya kutekeleza dini yao.
Hii ni ziara ya pili ya Benedikt nchini Ujerumani tokea alipochaguliwa kushika wadhifa huo wa Upapa mwaka jana.