Merz: Mazungumzo ya biashara ya Ulaya na Marekani ni magumu
23 Juni 2025Matangazo
Amesema Kamisheni ya Ulaya, ambacho ndicho chombo kikuu kinachojadili kuhusu makubaliano ya kibiashara ya mataifa 27 yanayounda Umoja huo, sasa kinapaswa kuangalia upande wa biashara ya magari, kemikali na dawa.
Rais wa Marekani Donald Trump alikuwa ametangaza ongezeko la asilimia 50 la ushuru kwa washirika wake wa kibiashara na kutaka kupunguza nakisi ya biashara ya bidhaa za Marekani na Ulaya.
EU kuweka shinikizo la kuondoa ushuru mpya wa Trump
Umoja wa Ulaya unawania kufikia makubaliano na Marekani kabla ya muda wa mwisho uliowekwa wa tarehe 9 Julai.