Siasa za uchaguzi nchini Kenya zimeanza kushika kasi kabla ya kufanyika 2022. Kikubwa zaidi ni kushuhudiwa kwa muungano kati ya vyama vya upinzani na chama tawala cha Jubilee. Je, upinzani unapoteza nguvu yake nchini Kenya? DW imezungumza na kiongozi wa chama cha upinzani cha ANC, Musalia Mudavadi, kutaka kujua zaidi.