Mashambulizi ya Urusi yawajeruhi wengi Kharkiv
7 Julai 2025Maafisa nchini Ukraine wamesema mtu mmoja ameuwawa na wengine 71 wamejeruhiwa baada ya Urusi kuushambulia mji wa Kaskazini mwa Ukraine wa Kharkiv wakati rais Volodymyr Zelenskiy akitoa wito wa msaada zaidi kutoka kwa washirika wa Ukraine.
Meya Ihor Terekhov amesema droni aina ya Shahed zilirushwa katika mji huo wa pili kwa ukubwa nchini Ukraine zilizolenga maeneo ya watu na miundombinu. Amethibitisha kujeruhiwa kwa watu 71 wakiwemo watoto saba.
Mashambulizi kati ya Urusi na Ukraine yasababisha kusitishwa safari za ndege
Kharkiv imekuwa ikilengwa mara kwa mara tangu Urusi ilipoanzisha uvamizi kamili wa kijeshi Fenbruari 2022.
Moscow imekanusha kushambulia makaazi ya watu lakini imekiri kushambulia miundo mbinu ya Ukraine inayoiwezesha kuishambulia nchi yake. Haya yanajiri wakati rais Vlodmy Zelensky akiwaomba washirika wake kuipa silaha zaidi ili kuimarisha ulinzi wake.