Mtu mmoja amekufa katika maporomoko ya ardhi China
9 Februari 2025
Matangazo
Watu wapatao 30 hawajulikani waliko. Vyombo vya habari vya serikali vimeripoti kwamba waokoaji wapatao 900 wanashiriki katika zoezi la kuwatafuta watu waliopotea. Maporomoko hayo ya ardhi yalikumba kijiji cha Jinping katika jiji la Yibin mwendo wa saa tano asubuhi. China imekumbwa na hali mbaya ya hewa katika miezi ya hivi karibuni, na mamia ya watu walikufa katika mafuriko mwaka jana. Wanasayansi wanasema mabadiliko ya hali ya hewa ndio chanzo cha maafa yanayotokea mara kwa mara nchini China. Rais Xi Jinping ameamuru mamlaka kufanya kila linalowezekana na kushughulikia ipasavyo maafa hayo.