Maandamano ya kupinga serikali yapamba moto Kenya
7 Julai 2025Matangazo
Waandamanaji waliwasha moto na kuwarushia mawe polisi huku maafisa hao pia wakiwarushia gesi za kutoa machozi na kumjeruhi mmoja ya waandamanaji.
Vijana wa kenya walipanga kufanya maandamano Julai 7 kulalamikia ukatili wa polisi dhidi yao, rushwa, uchumi mbaya, kupanda kwa gharama ya maisha na kumtaka pia rais William Ruto kuondoka madarakani.
Watu wanne wameuawa nchini Kenya
Julai 7 ni siku ya kihistoria nchini Kenya inayojulikana kama 'Saba-Saba' inayoadhimisha sasa miaka 35 ya kuwakumbuka waliopigania demokrasia na mfumo wa vyama vingi nchini humo mwaka 1990, baada ya kupitia miaka mingi ya utawala wa kiimla kutoka kwa rais wa wakati huo Daniel Arap Moi.