JangaUturuki
Mtu mmoja afariki kufuatia tetemeko la ardhi nchini Uturuki
11 Agosti 2025Matangazo
Mamlaka ya usimamizi wa majanga ya Uturuki (AFAD) imesema tetemeko hilo lilitokea majira ya saa moja na dakika 53 usiku wa Jumapili na kitovu chake ilikuwa katika mji wa Sindirgi, na kwamba shughuli za uokoaji sasa zimekamilika na hakuna dalili za uharibifu mkubwa.
Hata hivyo Waziri wa Mambo ya Ndani wa Uturuki Ali Yerlikaya amesema majengo 16 yameporomoka kutokana na tetemeko hilo lililosikika hadi katika mji wa Istanbul unaopatikana karibu kilometa 200 na mkoa huo wa Balikesir.