Mtu mmoja afariki kwa ugonjwa wa Ebola Uganda
31 Januari 2025Katibu mkuu wa wizara hiyo, Diana Atwine, amekiri mbele ya waandishi wa habari kuwepo kwa mripuko wa virusi vya Ebola baada ya maabara tatu za taifa kuthibitisha.
Wizara ya Afya ya Uganda imesema kuwa muuguzi aliyekufa kwa Ebola ni mwanamume mwenye miaka 32, mwajiriwa wa hospitali ya rufaa ya Mugalo, aliyeanza kupata dalili zinazofanana na za homa.
Soma pia: Sierra Leone kuzindua kampeni ya chanjo dhidi ya Ebola
Taarifa hiyo iliyotolewa kupitia jukwaa la X imesema viungo vya ndani ya mwili wa muuguzi huyo vilishindwa kufanya kazi na hatimaye kufariki dunia.
Imeongeza kuwa hakuna mhudumu mwingine wa afya au mgonjwa aliye wodini ambaye ameonesha dalili za Ebola. Wizara hiyo ya afya ya Ulinzi ya Uganda imesema timu za dharura za kukabiliana na maambukizi zimesharatibiwa.