Mtu mkongwe zaidi duniani afariki dunia akiwa na miaka 116
4 Januari 2025Taarifa ya meya wa mji huo wa kusini mwa Japan imesema Itooka, ambaye alikuwa na watoto wanne na wajukuu watano, alifariki Desemba 29 mwaka jana katika nyumba ya wazee ambako aliishi tangu mwaka wa 2019.
Bi Itooka alizaliwa Mei 23 mwaka 1908 katika kitovu cha kibiashara cha Osaka, karibu na Ashiya. Ajuza huyo alitambuliwa kuwa mtu mkongwe zaidi duniani na Kitabu cha Rekodi za Dunia cha Guinness baada ya kifo cha Mhispania Maria Branyas Morera mnamo Agosti mwaka 2024 akiwa na umri wa miaka 117.
Itooka, ambaye alikuwa mmoja wa watoto watatu kwenye familia yake, aliishi na kuviona vita viwili vikuu vya dunia na majanga ya magonjwa ya miripuko pamoja na mafanikio ya kiteknolojia. Kwa mujibu wa taarifa ya meya wa Ashiya, Itooka alipenda kula ndizi na kinywaji chenye maziwa ambacho ni maarufu nchini Japan.