Huko nchini Tanzania baadhi ya wabunge wamezusha mjadala mkubwa baada ya kutoa matamshi hadharani ya kutaka polisi itumie nguvu kubwa kuwakabili raia na wanahakarati kutoka nje wanaopaza sauti kuhusu hali ya demokrasia kwenye taifa hilo la Afrika Mashariki. Mchambuzi wa siasa za Tanzania Marcel Hamdun ameelezea nini huenda kimechochea matamshi ya aina hiyo.