You need to enable JavaScript to run this app.
Nenda kwenye maudhui
Nenda kwenye orodha kuu
Nenda tovuti zaidi za DW
Vidio zetu
Sauti zetu
Maeneo
Tanzania
Kenya
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo
Afrika
Ulaya
Mada
Haki za binadamu
Mazingira
Afya
Teknolojia
Kategoria
Matukio ya Kisiasa
Masuala ya Jamii
Michezo
Yanayoangaziwa
Mzozo wa Kongo Mashariki
Mzozo wa Israel na Hamas
Bundesliga
Sauti zetu
Vidio zetu
Matangazo
Msichana Jasiri
Kila msichana ana nafasi sawa kuwa jasiri - Msichana Jasiri!
Ruka sehemu inayofuata Maudhui yote kwenye mada hii
Maudhui yote kwenye mada hii
Rahma: Jasiri katika kupambania mazingira bora
Kila kukicha athari za mabadiliko ya tabia nchi zinashuhudiwa ulimwenguni kote, ikiwemo joto kuongezeka, mafuriko, mvua sizizo za wakati na wakati mwingine kiangazi kinachosababisha ukame mkali, lakini jambo la kutia matumaini ni kwamba wapo watu wanaotoa elimu ili kushirikiana kukabili changamoto hii ya ulimwengu. Rahma ni miongoni mwao na ndio mgeni wetu kwenye Msichana Jasiri leo
Mapambano ya kiuchumi kwa wasichana na wanawake
Kumuandaa mwanamke wa baadae ni kumuwekea mazingira bora msichana katika kila sekta ili kufikia malengo ya kujitegemea kiuchumi kwenye azma ya kuupiga kumbo umasikini inapofika 2030, lakini kutimiza hilo ni muhimu kumjumuisha kila mmoja, wasichana nao hawajabaki nyuma katika mbio hizo. Ungana na Mitchelle Ceasar katika video ya Msichana Jasiri.
Msichana Jasiri yamuangazia Naishooki Gideon, mhamasishaji
Ongezeko la ukatili wa kijinsia ulimsukuma kuwa mhamasishaji na muelimishaji wa vijana katika jamii. Mtangazaji wetu chipukizi Mitchelle Ceaser anaangazia juhudi zake Naishooki Gideon kwenye vidio yetu ya Msichana Jasiri
Mary Angel: Sanaa na muziki nyenzo za elimu ya afya ya akili
Sanaa ni nyezo ambayo hutumika katika kufikisha ujumbe kwa hadhira katika njia tofauti ikiwemo muziki, uchoraji na hata ufinyanzi na katika matumizi haya hapa ndipo anajitokeza msichana ambaye anaamua kuitumia sanaa ya muziki pamopja na uchoraji katika kuelimisha juu ya afya ya akili je nikwanini aliamua kutumia sanaa katika kuelimisha na elezea hisia binafsi? Jua mengi kupitia Msichana Jasiri.
Wasichana wachukua mwelekeo mpya wa ngoma za asili
Licha ya kutawala kwa muziki na midundo ya kisasa ambayo inawapagawisha watu wengi, lakini bado ladha ya ngoma za asili zimebaki kuwa pendwa miongoni mwa wengi. Wasichana wa kundi la Shine wanajifua kuunga'arisha muziki huo na kuutegemea kama ajira katika maisha yao ya baadae.
Msichana Jasiri: Watetezi wachanga wa haki za binadamu
Adeline Adelhard na Adela Adelhard ni dada pacha. Kando na kufanana kwa muonekano pia wanafanana kwenye mitazamo na maono yao. Si ajabu katika umri wa miaka 13, tayari wanatetea haki za watoto nchini Tanzania. Ndio wanatupambia makala ya Msichana Jasiri leo wakiwa Dar es Salaam. Mwenyeji wao ni mtangazaji chipukizi Mitchelle Ceaser
Kutana na mbunge kijana wa Tanzania katika bunge la SADC
Makala ya Msichana Jasiri leo inamuangazia kijana mwakilishi wa Tanzania katika bunge la Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika SADC Meseline Raphael. Je alifikaje huko? Milima na mabonde anayokutana nayo ni kama yapi? Je ni vipi amekuwa mfano kwa vijana wenzake, na ndoto yake kuu ni ipi? Mtangazaji wetu chipukizi Mitchelle Ceasar amezungumza naye. Tazama.
Leticia Shija msichana jasiri wa Dar es Salaam
Leticia Shija, binti mdogo mwenye faida kubwa kwa vijana na hasa wasichana wenziwe. Mtazame, msikilize katika mazungumzo yake na Mitchelle Ceasar mtangazaji chipukizi wa DW.
Sanaa ya kuchora na musiki katika kuokoa wasichana
Sanaa ya muziki inapitisha ujumbe kwa namna nyepesi kabisa miongoni mwa vijana, Je wasanii wanawakumbuka shabiki zao?
Nyota changa inayong'ara katika sanaa ya uigizaji Tanzania
Nyota inang'ara katika sanaa ya uigizaji kwa msichana mdogo Samira, wazazi wamekuwa na mchanga katika safari yake.
Ummi Sadick, msichana jasiri anayeongoza kampeni ya afya
Kutana na Ummi Sadick, msichana anayeongoza kampeni ya afya ya jamii mjini Mombasa, pwani ya Kenya.
Msichana Jasiri: Mfahamu Ahlam Swaleh, binti anayewasaidia vijana kuleta mabadiliko
Ni binti aliyejitokeza kuwasaidia vijana wenzake kuleta mabadiliko kupitia mpango wa ushauri kwa wanafunzi. Ni binti wa miaka 24 tu, lakini tayari ananuia kufanya mabo makubwa sana katika kuwainua wenzake huko pwani ya Mombasa nchini Kenya. Ni nani huyu? Ungana na Fathiya Omar kumfahamu zaidi kupitia makala haya ya msichana Jasiri.
Mfahamu Mai Zumo msichana muigizaji
Mai Zumo alingia kwenye sanaa ya uchekeshaji akiwa na miaka mitatu, safari yake ilianza bila ya kutaraji.
Msichana Jasiri inamuangazia dada mjenzi Dar es Salaam
Recho ni msichana aliye amua kuipigania kesho yake licha ya baadhi ya watu kuwa na mtazamo tofauti juu yake lakini haikuwa sababu ya yeye kutokufika hapa alipo. #MsichanaJasiri
Msichana Jasiri: Unaitumiaje mitandao ya kijamii?
Katikati ya changamoto zinazotokana na matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii, nchini Tanzania anajitokeza binti huyu ambaye anawasaidia wengi kutambua ya kwamba mitandao hii si ya kupotezea muda, bali ina faida. Ni kwa namna gani? Ungana na Tatu Yahya anayetukutanisha na binti huyu katika makala ya Msichana Jasiri.
Msichana Jasiri: Wachezaji chipukizi wa mpira wa kikapu
Michezo sasa imegeuka fursa kwa vijana na hata wasichana pia hawajabaki nyuma katika kuitumia michezo kukutana na watu na kufika mbali zaidi, licha ya kuwa na changamoto katika michezo na jamii kuwa na mtazamo mbaya juu yao, lakini si sababu ya wao kutokuziishi ndoto zao. Je wamefanikisha katika hili?
Msichana Jasiri: Binti mwandishi wa vitabu
Ni binti mdogo sana, lakini tayari anaandika vitabu vyake anapokwenda safari mbalimbali. Ni nani huyu hasa? Ungana na Hadija Halifa aliyemtembelea binti huyu. Utafurahi kumsikiliza. #msichanajasiri
Msichana Jasiri, aliyerejea shule baada ya kujifungua
Huyu ndio tunamuita msichana jasiri. Hakutaka kuacha ndoto yake ipeperuke, akatumia fursa iliyotolewa na serikali ya Tanzania na kuamua kurudu shuleni baada ya kujifungua. Ni nani hasa msichana huyu? Sikiliza makala ya Msichana Jasiri kujua zaidi.
Dora jasiri anaetumia tamthilia kuelimisha juu ya unyanyapaa
Baada ya kutengwa na kunyanyapaliwa na jamii kutokana na maumbile yake, Dora ameamua kutumia filamu kuelimisha jamii kwa njia ya Filamu na tamthilia nchini Tanzania.
Msichana Jasiri: Binti Mwandishi wa Vitabu
Katika umri wa miaka nane tu anaandika, vitabu kuhusu utalii wa Tanzania pamoja na utunzaji wa Mazingira
Mpira wa kikapu kwa wasichana wageuka fursa
Licha ya kuwa na changamoto katika michezo na jamii kuwa na mtazamo mbaya juu yao, lakini si sababu ya wao kutokuziishi
Kundi la wasichana na sanaa ya uoni
Hii ni sanaa ya kufikirika kwa kutumia picha halisia na zile za kubuni na rangi. Kundi hili linatumia sanaa hiyo ngumu k
Mabaki ya vifungashio hadi mapambo ya ndani
Modesta Oguda hutumia visoda, mabaki ya chupa na hata vifuu vya nazi kutengeneza mapambo na bidhaa nyengine. Modesta anatamani kuwa na kiwanda kikubwa ili kutoa ajira zaidi kando na kutangaza utamaduni wa kiafrika duniani.Ungana na Hadija Halifa
Msichana Jasiri: Sharon Ringo Balozi wa Utalii Afrika Mashariki
Msichama Jasiri: Sharon Ringo Balozi wa Utalii Afrika Mashariki
MSICHANA JASIRI: Msichana aliyeachana na fani ya Sayansi na kugeukia ufundi wa viatu
Taaluma aliyoichagua na kuisomea chuoni ni ukemia, lakini changamoto ya ajira imempa sababu ya kugeukia ubunifu wa viatu na kuachana na sayansi. Je kwa kiwango gani anafurahia tasnia hiyo na kuwa kioo kwa wasichana wengine? Makala ya Msichana Jasiri inamuangazia Amina Mohammed.
Msichana Jasiri-Asia Mussa , binti wa mjini anayefanya ufundi wa magari
Wahenga walisema mchagua jembe si mkulima, na kazi ni kazi mradi mkono uende kinywani. Binti Asia Mussa wa Dar es Salaam ameamua kuwa badala ya kukimbizana na kazi za kuajiriwa, afuate ndoto zake, akakunja mikono ya shati na kuzamia katika umakenika wa magari. Na huo ni mwanzo tu. Sikiliza hadithi yake, na pia ndoto zake katika vidio hii ya #MsichanaJasiri.
Msichana Jasiri: Mfahamu Madeeha Ghulam na harakati zake
Maddeha Ghulam ni binti anayemulikwa safari hii kwenye makala hii maalumu kabisa ya wasichana wanaoamua kuchukua hatua za kuisaidia ama kuinusuru jamii na mengine yanayozunguka jamii hizo. Ni nani hasa huyu bintiß Sikiliza makala haya.
Msichana wa miaka 13 anamiliki kiwanda cha sabuni
Umri si kigezo cha uthubutu haya yanadhihirishwa na msichana mgogo aliyejifunza ujasiriamali na bidhaa zake zipo sokoni
Msichana Jasiri kutoka Marsabit, Kenya
Katika kipindi cha Msichana Jasiri, Michael Kwena anamuangazia Jillo Fugicha, Msichana Jasiri kutoka Marsabit, nchini Kenya ambaye ameanzisha Shirika la kijamii la kupambana dhidi ya Ukeketaji.
Jasiri anaeamini juu ya elimu ya mazingira kwa jamii
Si kila mmoja anaweza kuthubutu kuhusu kuyatunza mazingira lakini kwa jasiri Upendo amethubutu zaidi kwa kuamini elimu pekee ndio suluhisho la kudumu katika kuyatunza mazingira na si elimu tu, bali kuwaelimisha watoto na wanawake kuhusu mazingira bora na ustawi wake.
Msichana Jasiri: Mtafsiri wa lugha ya alama
Makala hii ya Msichana Jasiri inamwangazia Halima Salim, binti anayejitolea kutafsiri lugha ya alama kwa wanafunzi wenzake ambao ni viziwi kwenye shule ya sekondari ya Mtwara Ufundi iliyoko mkoani Mtwara kusini mwa Tanzania. Msikilize Salma Mkalibala akisimulia.
Msichana Jasiri: Msichana anayetoa elimu shuleni na vyuoni juu ya kujitambua
Katika umri wa miaka 19 tu swaiba anathubutu kupita shuleni pamoja na vyuoni kuitoa elimu kwa wasichana wengine juu ya kujitambua. Hii si rahisi kwake lakini nguvu nyingi na masaada wake mkubwa unatoka katika jamii. Si rahisi kwa jamii yake kumuelewa lakini matumaini yake ni kuwafikia wasichana wengi na anatamani kuona wazazi wanaotoa elimu madhubuti juu ya kujitambua kwa vijana wao.
Msichana Jasiri: Rubani ambaye pia anatengeneza udi
Wadh- hat ni rubani ambaye ameamua kuwafundisha watu jinsi ya kutengeneza udi ili kujikwamua na janga la ukosefu wa ajira. Kwake haikuwa rahisi kwa sababu watu wa jamii yake waliamini kuwa udi bora hutoka katika mataifa ya Uarabuni. Lakini sasa amekuwa ni msaada kwa baadhi ya watu na hata wengine kumuona kuwa daraja kwao katika kuyafikia malengo yao.
Wakonta anatumia ulimi,teknolojia kuandika
Ajali alioipata haikuzuia kufikia malengo yake ya masomo na biashara, alijifunza kutumia viungo vilivyobaki katika lengo
Jasiri katika kilimo biashara
Alipoanza kilimo biashara familia haikumuelewa lakini kadri alivyoamua kuongeza bidii katika kile anakiamini, sasa anafurahia hatua anazopiga. Anamiliki kiwanda kidogo kuchakata viungo vya kupikia
Fahamu ndoto za Witness Raphael mlimbwende wa viti mwendo
Msichana aliyethubutu kuwania mashindano ya ulimbwende wa viti mwendo Duniani , safari yake haikuwa rahisi lakini uthubutu wake umekuwa na manufaa na kuwa mfano kwa wasichana na vijana wengine. Anatamani kuona jamii yenye usawa haswa kwa watu wenye changamoto za kimaumbile kujitokeza na kutumia vilivyo vyao ili kuziishi ndoto zao.
Jasiri kwa wasio na makaazi
Ayshat msichana anayelikusanya kundi la watoto lililosahaulika na kuwapatia mahitaji yao muhimu huku akiwa akitamani kuona jamii yenye usawa na anatamani kuona jamii inalikumbuka kundi hili.Tazama video
Mfahamu msichana anayeelimisha jamii kwa kutumia vitabu
Msichana wa miaka 16 anaielimisha jamii kwa kutumia vitabu huku akiwa na changamoto ya kifedha kwaajili ya kuchapisha kitabu chake ana imani kuwa watu wengi wataelimika kwa kupitia utunzi wake huku akizitoa fikra potofu juu ya msichana anayafanya haya yote akiwa na matarajio makubwa juu ya msichana katika jamii anatamani kuona jamii yake inaitambua thamani ya msichana. #MsichanaJasiri
Je, unaweza kukuza talanta ya Karate kwa mtoto wa kike?
Je, unaweza kukuza talanta ya Karate kwa mtoto wa kike?
Jasiri wa Dar es Salaam Asia Matona
Jasiri wa Dar es Salaam Asia Matona
Ubunifu unalipa..!!!
Sammy Julius si tu ni msichana aliyeitumia changamoto na kuwa fursa. Bali pia amefanikiwa pakubwa na sasa anakuwa miongoni mwa waajiri nchini Tanzania. Anafanya nini hasa? Tizama video hii ya msichana Jasiri. #Msichanajasiri
Kutana na Jane Limwata, kijana mhamasishaji
Yeye ni kati ya kina dada wachache ambao hujitolea kuwa wanaharakati kwa lengo la kuhamasisha umma. Je Jane Limwata anatekeleza majukumu yake vipi na kukabiliana na changamoto dhidi yake? Hadija Halifa anayatafutia majibu kwenye #MsichanaJasiri
Msichana Jasiri: Mhelepu Shilingi atumia sanaa kujiajiri
Mhelepu Shilingi ni msichana ambaye amefanikiwa na kuziishi ndoto zake kwa sanaa yake ya uchoraji. Amefanikiwa kuwafundisha watu wengine na pia amepata tuzo ya msichana anayezipambania ndoto zake. Matamanio yake ni kuona vijana wanathubutu katika kuziishi ndoto zao.Mwandishi wetu chipukizi Hadija Halifa alimtembelea miaka miwili iliyopita na sasa amerudi tena kuona mafanikio yake.
Changamoto za wasichana zimetatuliwa Tanzania?
Juma hili dunia imeadhimisha siku ya Mtoto wa kike huku bado changamoto lukuki zinamtaza, lakini walau sasa kuna jitihada zinaonekana.Tazama video na Hadija Halifa, je malengo dunia inayotaraji yamefikwa?
Kutana na wacheza ala za muziki chipukizi
Mpambanaji ustawi afya ya akili kwenye jamii
Hali ya matukio ya kutisha kwenye jamii yanampa sababu ya kupambania kizazi kijacho kwa kutoa elimu ya afya ya akili
Msichana Jasiri:Unaitumiaje mitandao ya kijamii?
Neema Kaniki ni msichana anayeitoa elimu juu ya mitandao ya kijamii licha ya kuwa baadhi ya wasichana wamebaki na alama mbaya anakuwa sehemu ya kuwaelimisha na kuitumia mitandao kwa faida na kuzikamata fursa zinazopatikana mitandaoni anatamani kuwafikia vijana wengi ili wanufaike na elimu anayoitoa.
Msichana anayetumia taka ngumu kubuni mavazi
Anakuja na taswira mpya katika tasnia ya ubunifu anapoamua kuzitumia taka ngumu haswa mifuko viroba katika kubuni mitindo mbali mbali ya mavazi japo si rahisi katika jamii yake kuamini katika hili lakini anakuwa mfano wa kwanza katika kuutambulisha ubunifu wake. Anatamani kuona anafanya makubwa katika tasnia ya mitindo na ubunifu. Huyu ni Nyeusi Yalami,#msichanajasiri
Qayllah msichana mwenye ndoto za kuwa rais
Msichana mdogo mwenye ndoto ya kuwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania anaamua kuuvaa uhusika na kuwahamasisha watu kuhesabiwa Na kuwatoa imani potofu juu ya hilo. Huku matamanio yake makubwa ni kuona watoto wanapata haki zao za msingi. #Kurunzi
Bahati jasiri katika michezo ya watoto
Bahati simba Katikati ya harakati zake analikusanya kundi la watoto wanaotoka katika mazingira mabayo si rafiki na kuwapa kile ambacho ni adimu katika mazingira yao ili nao wafikie matafanikio kwenye sekta ya michezo.
Ukurasa uliotangulia
Ukurasa 2 wa 4
Ukurasa unaofuatia