You need to enable JavaScript to run this app.
Nenda kwenye maudhui
Nenda kwenye orodha kuu
Nenda tovuti zaidi za DW
Vidio zetu
Sauti zetu
Maeneo
Tanzania
Kenya
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo
Afrika
Ulaya
Mada
Haki za binadamu
Mazingira
Afya
Teknolojia
Kategoria
Matukio ya Kisiasa
Masuala ya Jamii
Michezo
Yanayoangaziwa
Mzozo wa Kongo Mashariki
Mzozo wa Israel na Hamas
Bundesliga
Sauti zetu
Vidio zetu
Matangazo
Msichana Jasiri
Kila msichana ana nafasi sawa kuwa jasiri - Msichana Jasiri!
Ruka sehemu inayofuata Maudhui yote kwenye mada hii
Maudhui yote kwenye mada hii
Msichana Jasiri: Loistracy Andrew na athari za ukeketaji
Msichana Loistracy atumia sauti yake kukabiliana na athari za ukeketaji. Matumaini yake ni kuwa sauti ya mabadiliko
Msichana aliyegeukia useremala licha ya kusomea diplomasia
Huyu ni msichana anayesoma diplomasia lakini pia anajivunia kuwa fundi selemara.
Msichana anayepiga vyombo vya muziki
Caren ni msichana wa miaka 10, lakini sauti na midundo yake ni mikubwa kuliko umri wake. Anapiga vyombo vya muziki na pia huimba kwa ustadi mkubwa. Ameshawahi kutumbuiza katika matamasha makubwa, na hata kutunukiwa cheti cha muziki. Bado ana ndoto ya kuliiwakilisha taifa lake katika majukwaa makubwa ya kimataifa kupitia muziki.
Msichana anayeongoza watalii majini
Kutoka kwenye pwani ya Tanzania hadi kwenye kina cha bahari, amegeuza hofu kuwa ujasiri na ndoto kuwa kazi.
Msichana anayetumia taka za plastiki kubuni bidhaa
Sarafina ni msichana mbunifu anayetumia taka za plastiki kubuni bidhaa.
Buminganyikani, msichana mdogo anayewasaidia wenzake
Buminganyikani ni msichana wa kidato cha sita ambaye amekuwa akitumia muda wake katika kutembelea vituo vya watoto.
Msichana Jasiri: Faith na uthubutu wa kuongea na umati
Kutana na Faith Fransis binti wa miaka 8 alojipatia umaarufu mitandaoni kwa kujieleza mbele ya umati.
Binti aliyejitosa kutunza mazingira Tanzania
Msichana jasiri wiki hii inamulika juhudi zinazofanywa na binti Ilakiza katika uhamasishaji wa kutunza mazingira nchini Tanzania. Anawaelemisha vijana wenzake kuhusu athari za mabadiliko ya tabianchi, uchafuzi wa mazingira, na umuhimu wa kuhifadhi vyanzo vya maji na misitu. #msichanajasiri #vijana #mazingira #tabianchi #tanzania
Uganda:Mjue kinda wa muziki wa "rap" nchini Uganda
Uganda:Mjue kinda wa muziki wa "rap" nchini Uganda
Uthubutu wa kuanzisha jukwaa la vijana mtandaoni
Doricas ni msichana wa miaka 20 ambaye ameanzisha jukwaa la kuwakutanisha vijana kuanzia miaka 15–25.
Msichana Jasiri: Mwanzilishi wa programu ya afya ya Akili
Adila Nassoro wa Tanzania aliamua kuanzisha programu ya kipekee dhidi ya unyanyapaa wa afya ya akili
Msichana Jasiri: Ijumaa Kuu
Wasichana wazungumzia umuhimu wa siku ya Ijumaa Kuu
Kutana na msichana anayepiga vita rushwa ya ngono
Joanitha ni mwanafunzi anayesomea masuala ya ustawi wa jamii. Anapinga masuala ya rushwa ya ngono kwa wasichana.
Taaluma yako inaweza kulinda afya ya jamii?
Faraja kama lilivyo jina lake, anayo ari na dhamira ya kweli ya kuleta mabadiliko katika jamii kupitia elimu ya afya. Akiwa mwanafunzi wa udaktari, ametumia maarifa anayoyapata chuoni kuelimisha jamii kuhusu magonjwa yasiyo ya kuambukiza ambayo yanachangia idadi kubwa ya vifo vya watu duniani.
Wasichana na matumizi ya Akili Bandia
Ni wasichana watatu walioamua kuwaelimisha wengine namna ya matumizi ya akili bandia katika kutafuta suluhu za changamot
Msichana Jasiri: Shadya Kitenge, mbunge wa viti maalum UDSM
Shadya kitenge ni mbunge wa viti maalum katika chuo kikuu cha Dar es Salaam. Shadya amekuwa katika mstari wa mbele kuwahamasisha wasichana wenzake kujiamini na kuthubutu kuwania nafasi za uongozi. Amekuwa alama na ushawishi kwa wasichana wengine kutamani kuwania nafasi za uongozi mbali na chuo.
Wasichana wajiandaa na sikukuu ya Eid
Zimesalia siku chache waumini wa dini ya kiislamu kukamilisha ibada muhimu ya funga, inayofuatiwa na shamrashamra za sikukuu ya Eid. Wasichana wamejipanga kusherehekea siku hiyo kwa namna gani?
Rozy: Kutoka mwanajeshi idara ya vilipuzi hadi makanika
Kama wasichana wengine wenye ndoto ya kuwa watu wa kutegemewa kwenye mataifa yao, alitamani kuwa mwanajeshi kwenye idara ya vilipuzi lakini mambo hayakuwa upande wake na kujikuta kwenye taaluma ya magari kama makanika. Hapo anatamani pia kufungua karakana itakayowaajiri wasichana na wanawake tu.
Rebecca: Msichana aliyegundua programu ya kuchagua vyuo
Rebecca ni msichana aliyebuni programu tumizi kwa ajili ya kuwasidia watu kuchagua vyuo kutokana na ufaulu. Programu hii inalenga kuwasaidia wanafunzi na watu wanaotaka kujiunga na vyuo vikuu kutafuta fursa kulingana na matokeo yao. #msichanajasiri
Msichana Jasiri - Sarafina Simioni - Mwanaharakati wa Jinsia
Katika jamii inayotawaliwa kwa sehemu kubwa na mfumo dume, inahitaji ujasiri wa kipekee kusimama na kutetea haki za wanawake na wasichana. Sarafina Simioni, binti mdogo lakini mwenye sauti kubwa, ni miongoni mwa mashujaa wa zama hizi. Ni mwanaharakati shupavu wa masuala ya jinsia nchini Tanzania, anayejituma kuelimisha na kuhamasisha jamii kuhusu haki za wanawake na wasichana.
Mfahamu Lina msichana muelimishaji juu ya hedhi salama
Elimu yake inawasaidia kujenga ujasiri, kuwa na afya bora, na kuwa na uelewa wa haki zao za kimwili.
Msichana Jasiri: Fursa katika dansi la mtaani
Dansi ni moja ya fursa kwa vijana wa dunia ya sasa, kundi la washichna wadogo kutoka jiji kuu la kibiashara Tanzania, Dar es salaam, wameanzisha kundi lao kwa ajili ya kunoa talanta na kusaka fursa hizo kupitia majukwa ya kidigitali.
Jackline Malavanu: Mtunzi wa Mashairi
Jackline Malavanu ni mtunzi mahiri wa mashairi anayejulikana kwa ustadi wake wa kipekee wa kutumia maneno.
Mfahamu nyota chipukizi katika filamu Tanzania
Najma Juma ni mwigizaji anayechipuka kwa kasi katika tasnia ya filamu. Kwa kipaji cha kipekee na juhudi zisizo na kikomo, amekuwa akivutia macho ya watazamaji na wataalamu wa filamu. Ingawa ni mpya kwenye tasnia, licha ya juhudi zake amekuwa akikumbana na changamoto kubwa ya kukatishwa tamaa katika mitandao ya kijamii lakini kwake anaitumia kama chachu ya kufikia malengo yake.
Msichana Jasiri: Kiongozi wa wanafunzi wenye mahitaji maalum
Safari ya viongozi wa ulimwengu huanzia mbali sana. Katika #msichanajasiri wiki hii, tunamwangazia Zainab Masoud kiongozi wa wanafunzi wenye mahitaji maalum katika chuo Kikuu Cha Ustawi Wa Jamii, kilichoko Dar es salaam Tanzania.
Jasiri katika kutetea viumbe wa baharini
Mabadiliko ya sayari yamesababisha changamoto kubwa katika bahari, hata baadhi ya viumbe wapo hatarini kutoweka kando na hilo uvuvi haramu ni changamoto nyingine inayotishia maisha yao, sasa kutana na Stella masai anatoa elemu kwa jamii ili kunusuru viumbe baharini.
Msichana Jasiri: Mhamasishaji juu ya elimu bora
Moureen ni msichana wa miaka 18 mwenye maono na ari ya kipekee, ambaye amejiweka mbele kama kiongozi katika kuhamasisha
Msichana Jasiri - Mwelimishaji vijana kupitia maandishi
Doroth ni binti aliyeandika kitabu. Mwandishi chipukizi Mitchelle Ceaser amekutana na Doroth kusikiliza maono yake.
Fahamu maudhui yanayowavutia wasichana mitandaoni
Wasichana wamekuwa na matumizi mbalimbali ya mitandao ya kijamii lakini wengi wao hukumbana na changamoto nyingi, ambazo wengine huwaachia alama mbaya, ni kipi hasa wanatakiwa kujifunza kabla ya kuingia katika ulimwengu wa kidijitali?
Msichana anayepigania kutokomeza ndoa za utotoni
Mamilioni ya wasichana kila mwaka huathirika na ndoa za utotoni ambazo zinawakosesha haki ya msingi ya elimu, matatizo ya afya ya uzazi pamoja na kukosa malezi ya wazazi wao. Hayo ni maneno ya Jenniffer Fred, mwanaharakati aliyeamua kulivalia njuga na kusambaza elimu ili kutokomeza ndoa za utotoni. Na huyu leo ndio #msichana wetu #jasiri. #msichanajasiri #hakizawatoto #hakiyaelimu
Mhamasishaji wa afya ya akili mitandaoni
Janeth ni msichana wa miaka 17 anayetumia mitandao ya kijamii kuwaelimisha vijana juu ya masuala ya afya ya akili na changamoto wanazokabiliana nazo. Japo vijana wengi hutumia mitandao, si wote ambao wanamuelewa. Lengo lake kuu ni kuona vijana wanatumia mitandao ili kuelimika na kufikia au kuzikamata nyadhifa mbalimbali.
Mfahamu msichana mwalimu wa biashara
Salma ni msichana wa miaka 22 ambaye amekuwa akiwafundisha vijana namna ya kuanzisha biashara na kuziendeleza. Hata hivyo, si rahisi kwa baadhi yao kumuelewa lakini bado anamatumaini makubwa ya kufikia kundi kubwa la vijana, ili kuhakikisha kuwa wanajikwamua katika ajira na kuishi katika ndoto zao. #msichanajasiri.
Mfahamu Dinales, msichana anayetoa elimu ya Tehama
Kutokana na idadi ndogo na muamko wa wasichana kujifunza juu ya tehema imekuwa sababu ya Dinales kuwafundisha wasichana wengine juu ya umuhimu wa tehama na matumizi ya teknolojia japo si rahisi kwa jamii kumuelewa lakini matamanio yake makubwa nikuona idadi ya wasichana inaongezeka katika kada hii kadhalika na uelewa mkubwa katika matumizi ya teknolojia.
Msichana anayeelimisha jamii kuhusu ukatili dhidi ya watoto
Kutokana na ongezeko la vitendo vya ukatili, Dolice amemua kutoa elimu ya kujikinga na ukatili kwa watoto hasa shuleni.
Mwandishi kinda wa vitabu vya utalii Tanzania
Katika umri wa miaka 9, Queen Florence tayari ameandika vitabu 2 vya kuhamasisha utalii uliojificha nchini Tanzania. Mojawapo ya kitabu chake amekipachika jina la “NCHI YANGU TANZANIA”. Na huyu leo ndio msichana wetu jasiri.
Mfahamu mlimbwende wa Vyuo Vikuu Tanzania
Latricia ni msichana ambaye amelitwaa taji la ulimbwende kwa vyuo vikuu Tanzania 2024, ambapo safari yake ya kuanza kuzifuata ndoto zake ilianza akiwa na miaka 16, kutokana na taji lake anatarajia kuwa msemaji wa wasichana huku akitarajia kuiwakilisha Tanzania katika mashindano ya urembo ulimwenguni. #msichanajasiri @latricia_ian12
Mtetezi wa watoto wenye usonji
Msichana Jasiri: Lembe binti wa Kitanzania wa mfano wa kuigwa katika juhudi ya utetezi wa watoto wenye usonji.
Msichana jasiri aliyejitosa fani ya kuchomelea vyuma
Katika umri wa miaka 19, Sharifa Karim amekuwa msichana hodari na jasiri katika fani ya uchongaji na uchomeleaji vyuma. Anasema haikuwa rahisi wakati alipoanza kutokana na fani hii kuwa na idadi kubwa ya wanaume lakini anaona ufahari kuifanya kazi hii. #msichanajasiri
Neema Athuman: Muigizaji mdogo wa Tanzania
Neema Athuman: Muigizaji mdogo wa Tanzania
Hedhi salama bado ni changamoto kwa wasichana
Hapo kabla ilikua ni nadra kulizungumzia suala la hedhi hadharani lakini muda inavyozidi mambo kuwekwa wazi hili linawapa nafasi wasicha kuzungumza suala hili kwa uwazi zaidi. #MsichanaJasiri
Wasichana wa sasa katika kuzienzi tamaduni zao
Katika safu yetu ya Msichana Jasiri, mjadala unaopewa nafasi unahusu. "Wasichana katika kuzienzi tamaduni zao."
Msomi wa uchumi na mbunifu wa mapambo ya ndani ya kitamaduni
Kutoka kuwa mwanauchumi mpaka kutumia stadi za mikono katika kujiajiri hii haikuwa rahisi kwake, lakini ule msemo waelimu ni ufunguo wa maisha kwake anautendea haki anaitumia elimu yake ili kuhakikisha kuwa anapata bidhaa zenye ubora na hata kuzitangaza kwa kutumia majukwaa mbalimbali huku akiwa na matarajio ya kufika katika soko la kimataifa.
Mwanaharakati wa haki za watoto wa mitaani Tanzania
Kundi la watoto wa mtaani ni kundi ambalo linaendelea kuongezeka kwa kasi huku watoto hawa wakiwa hawana elimu madhubuti kutokana na ukatili wanaokutana nao, lakini juhudi za wanaharakati wa masuala ya kijamii ni zipi katika kuhakikisha kuwa wanalisaidia kundi hili. Jackline Joseph ni mwanaharakati ambaye amejitolea katika kulisaidia watoto katika kuwapatia elimu dhidi ya ukatili.
Chipukizi wa muziki wa kizazi kipya
Precious ni mwanamuziki chipukizi wa kizazi kipya kutoka Tanzania ambaye Uwezo wake wa kutumbuiza katika majukwaa umempa sababu ya kuwa mfano kwa watoto wengine. Anasema baba yake ndiye aliyempa msukumo mkubwa wa kunoa kipaji chake. #msichanajasiri.
Wasichana wanavyosherehekea sikukuu ya Pasaka
Katika sikukuu ya pasaka kumekuwa na changamoto nyingi ambazo huwakuta wasichana pale wanapoenda kujivinjari katika viwanja tofauti tofauti lakini vipi wanaweza kuepukana na hayaWasichana wanavyosherehekea sikukuu ya Pasaka
Wasichana jitokezeni kwenye sayansi na teknolojia
Miriam ameona ombwe la wasichana kujitosa katika masomo ya sayansi, kwa nafasi yake mbali na kuwa katika masuala ya sayansi na teknolojia, lakini pia amekuwa muhamasishaji kwa wasichana wengine kujitokeza katika sekta hiyo.
Jasiri mwenye ndoto za kuwa mwanamasumbwi bora duniani
Kuingia kwake katika mchezo wa ngumi kuliambatana na changamoto nyingi lakini bado anaonesha ari kubwa katika kuziishi ndoto zake. Anatamani kuwa bondia mkubwa ulimwengu lakini ushirikiano anaoupata kutoka kwa watu wake umekua hafifu. Vipi anaweza kuzimudu changamoto hizi ili kufikia malengo yake?
Turakella: Ubaguzi nchini Algeria ulifungua mlango wa fursa
Akiwa katika safari yake ya elimu nchini Algeria msichana Turakella anakumbana na visa vya ubaguzi, ambavyo badala ya kumdhoofisha viligeuka fursa kwake na kuingia katika ulimwengu wa sanaa adimu. Sikia hadithi hii kupitia msichana jasiri
Leila Abdul Kheir na vita dhidi ya utoaji mimba holela
Jamii huepuka kuyajadili maswala ya wanawake hasa yanayohusiana na ujauzito na utoaji mimba kwani huchukuliwa kuwa aibu.
Binti Jasiri Magreth: Mwenye changamoto ya kusikia
Msichana Magreth Mathias ana changamoto ya kusikia lakini ameweza kuanzisha kampuni yake na kutoa ajira kwa wenzake. Mtazame katika vidio hii ya "Msichana Jasiri"iliyoandaliwa na Mitchelle Ceasar
Ukurasa uliotangulia
Ukurasa 1 wa 4
Ukurasa unaofuatia