Shadya kitenge ni mbunge wa viti maalum katika chuo kikuu cha Dar es Salaam. Shadya amekuwa katika mstari wa mbele kuwahamasisha wasichana wenzake kujiamini na kuthubutu kuwania nafasi za uongozi. Amekuwa alama na ushawishi kwa wasichana wengine kutamani kuwania nafasi za uongozi mbali na chuo.