Katika jamii inayotawaliwa kwa sehemu kubwa na mfumo dume, inahitaji ujasiri wa kipekee kusimama na kutetea haki za wanawake na wasichana. Sarafina Simioni, binti mdogo lakini mwenye sauti kubwa, ni miongoni mwa mashujaa wa zama hizi. Ni mwanaharakati shupavu wa masuala ya jinsia nchini Tanzania, anayejituma kuelimisha na kuhamasisha jamii kuhusu haki za wanawake na wasichana.