Ulipokuwa na miaka minane ulikuwa unaweza kujieleza mbele za watu? Au ulikuwa unajificha ficha ukiitwa mbele ya umati? Sasa msichana Faith Fransis amejizolea umaarufu mitandaoni huko Tanzania kutokana na ujasiri na umahiri kwa kusimama mbele ya umati na kujieleza.