Sarafina ni msichana mbunifu anayetumia vifuniko vya chupa za plastiki kutengeneza bidhaa mpya zenye manufaa kama vile mapambo ya nyumbani, ofisini na vikapu.
Kwa ubunifu wake, anasaidia kupunguza uchafuzi wa mazingira huku akihamasisha jamii kuhusu umuhimu wa kuchakata taka na kutumia rasilimali zilizopo kwa njia endelevu.