Mshauri wa Netanyahu huenda akashtakiwa
14 Julai 2025Matangazo
Msaidizi na mshauri wa karibu wa waziri mkuu wa Israel,Benjamin Netanyahu anakabiliwa na uwezekano wa kushtakiwa kuhusiana na makosa ya kiusalama. Jonatan Urich anatuhumiwa kuvujisha taarifa za siri za kijeshi wakati wa vita vya Israelkatika Ukanda wa Gaza.
Mshauri huyo wa karibu wa Netanyahu amekanusha kuhusika na makosa yoyote katika kesi hiyo ambayo mamlaka za kisheria nchini humo zilianza kuendesha uchunguzi tangu mwishoni mwa mwaka uliopita.
Netanyahu amesema uchunguzi dhidi yaUrichna wasaidizi wake wengine ni hatua iliyochochewa kisiasa na kwamba Urich hajasababisha madhara yoyote kwa usalama wa taifa.