Mshambuliaji timu ya taifa Gabon Aaron Boupendza amefariki
16 Aprili 2025Matangazo
Shirikisho la soka la Gabon (FEGAFOOT) limetangaza kifo hicho leo Jumatano.
Kupitia taarifa kwenye mtandao wa X, shirikisho hilo la soka la Gabon limeandika kuwa Boupendza atakumbukwa kama mshambuliaji maahiri aliyeacha alama ya kudumu katika michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika yaliyoandaliwa nchini Cameroon mwaka 2022.
Boupendza, aliyejiunga na klabu ya Zhejianga FC ya China mapema mwaka huu, alikuwa katika fomu nzuri ya mchezo kwa kufunga mabao manne katika mechi sita.
Mamlaka nchini China zimeanzisha uchunguzi kubaini iwapo kuanguka kwake ilikuwa ni ajali, jaribio la kujiua au tukio la uhalifu.