MSF yatoa lawama kwa shirika la misaada kwa machafuko Gaza
2 Juni 2025Shirika la misaada la madaktari wasio na mipaka MSF limesema kwamba watu waliowatibu katika eneo la misaada la Gaza linaloendeshwa na shirika jipya linaloungwa mkono na Marekani waliripoti "kupigwa risasi kutoka pande zote" na vikosi vya Israel.
MSF imelilaumu shirika hilo jipya kwa machafuko yaliyotokea wakati wa kutolewa kwa misaada katika eneo la mji wa kusini wa Gaza wa Rafah.
Katika hatua nyingine, shirika la ulinzi wa kiraia wa Gaza limesema mashambulio hayo ya Israel yamewaua Wapalestina 31 katika eneo hilo. Walioshuhudia wameliambia shirika la habari la AFP kuwa wanajeshi wa Israel waliwafyatulia risasi.
Hata hivyo, madai hayo yamekanushwa vikali na Israel pamoja na shirika jipya la misaada la GHF ambalo linaloungwa mkono na Marekani.